Wakati wanachama wengi wa jamii mbali mbali wana endelea kusita kupokea chanjo ya COVID-19, viongozi wa jamii yawatanzania wanao ishi Victoria, wame andaa mkutano maalum kwenye mtandao wa Zoom ambako wataalam wamaswala ya afya, wame alikwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu; uelewa wa COVID-19: virusi hivyo, chanjo, athari za afya ya akili pamoja na uzoefu tunao changia.
Habib Chanzi ndiye Rais wa Jumuia yawatanzania wa Victoria, ali eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS kuhusu umuhimu na lengo lakuandalia jamii yake mkutano huo. Tembelea ukurasa wa Facebook wa: Tanzanian Community of Victoria, kwa taarifa kuhusu jinsi yakushiriki katika mkutano huo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.