Kutegemea unako ishi nchini Australia, masharti yanatofautiana unapo uza gari ya matumizi binafsi.
Kuelewa hatua zinazo muhimu na mapendekezo katika mchakato mzima, kuanzia kwa kuandaa gari yako hadi kukamilisha mchakato waku iuza, kunaweza hakikisha uhamisho laini nawa kisheria wa umiliki.
Wakati hakuna mamlaka kitaifa inayo kusanya data ya mauzo ya gari, makadirio yanadokeza kuwa kiwango cha magari yaliyo tumiwa ni takriban mara tatu ya soko ya magari mapya nchini Australia.
Kama muuzaji wa gari lililo tumiwa, una idadi kubwa ya wateja ambao unaweza lenga. Ila, unawezaje kabiliana na mchakato waku uza gari yako?