Mjini Brisbane, Queensland maelfu yawatu walijumuika mitaani, kuandamana dhidi ya mauaji ya mmarekani mweusi George Floyd nchini Marekani.
Waandamanaji hao walipaza sauti zao pia wakita hatua zichukuliwe kwa vifo vya waaustralia wakwanza vizuizini. Mwanasheria Blaise Itabelo, alikuwa miongoni mwa watu walio shiriki katika maandamano hayo, alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS alivyo shuhudia.
Maandamano hayo yalijiri wakati, viongozi wakiwahamasisha watu kuto tangamana katika umma kwa ajili yakuzuia usambaaji wa virusi vya corona. Maandamano hayo yalihudhuriwa na idadi kubwa ya watu, kuliko maandamano mengine katika mji huo.