Scott Morrison na Anthony Albanese walipo tembelea maeneo bunge mhimu, mada za ulinzi wa mipaka na maswala ya huduma ya afya yalikuwa juu ya ajenda zao.
Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani walitembelea maeneo bunge mhimu jana Jumatatu. Scott Morrison akiwa Magharibi Australia ambako chama cha Liberal, kilishindwa vibaya katika uchaguzi wa jimbo hilo mwaka jana. Alitembelea pia eneo bunge la Pearce, ambalo lilikuwa chini ya uongozi wa mbunge anaye staafu Christian Porter. Hiyo ilikuwa ziara ya tatu ya waziri mkuu jimboni humo katika muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Wakati huo huo Anthony Albanese anajua anakazi ya ziada jimboni Queensland, ambako chama cha Labor kiliteseka sana katika uchaguzi mkuu uliopita. Katika wiki zijazo wawili hao wataendelea kutembelea maeneo bunge ambayo lazima vyama vyao vishinde katika uchaguzi mkuu.