GLAPD International ni shirika lisilo la faida ambalo hutoa huduma zake katika eneo la Kusini Magharibi ya Sydney.
Shirika hilo hutoa huduma kwa jamii kutoka mashariki na kati ya Afrika, moja ya huduma ambazo GLAPD International hutoa nikuwezesha mshikamano katika jamii kupitia matukio ya michezo.
Jamii yawa Kenya wanao ishi Sydney watashiriki katika tukio la michezo linalo andaliwa na GLAPD. Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na mwakilishi wa shirika la KISWA ambalo wanachama wake wanaishi katika maeneo ya magharibi Sydney. Mjumbe huyo alitueleza kuhusu umuhimu wa michezo kukuza ushikamano katika jamii pamoja na umuhimu wa michezo kwa mtu binafsi na jamii pana. Tukio hilo la michezo litakuwa tarehe 2 Novemba, katika ukumbi wa michezo wa Whitlam Leasure Centre, 90 Memorial Ave, Liverpool NSW 2170