Chama cha Liberal kime mchagua mweka hazina Scott Morrison, kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya wiki iliyo jawa, sintofahamu na usaliti katika siasa ya shirikisho.
Bw Morrison aliwania wadhifa wa kiongozi wa chama cha Liberal na Waziri Mkuu, dhidi ya aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani Peter Dutton na waziri wa maswala ya nje Julie Bishop, katika uchaguzi ulio fanywa na chama cha Liberal.
Je, waziri mkuu wa 30 wa Australia ni nani?
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanywa katika miezi tisa ijayo, Scott Morrison sasa lazima ashawishi taifa kuwa, chama cha Liberal ambacho kime onesha utulivu na uhakika mdogo, ndicho chama bora kinacho stahili ongoza taifa.
Share






