Jua linapo chomoza katika siku ya ANZAC, mlio unao fahamika wa tarumbeta huwaleta wa Australia na watu wa New Zealand pamoja kote nchini na duniani kuwakumbuka walio potezwa katika vita.
Ilikuwa miaka 107 iliyopita leo (Jumatatu 25 Aprili 2022) wanajeshi wa Australia na New Zealand walipo tua katika eneo la Gallipoli nchini Uturuki katika vita vya kwanza vya dunia. Wanajeshi hao wanao julikana kwa jina la ANZACs, walishindwa miezi minane baadae baada, yakukabiliwa kwa magumu mengi pamoja na majeruhi wengi.
Ibada hizo zilifuatwa na gwaride zamaveterani pamoja na shughuli zingine zaukumbusho kama ilivyo tamaduni. Ng’ambo, sherehe za ukumbosho zitafanywa nchini Ufuransa, Uturuki, Thailand, Malaysia, na Papua New Guinea.