Walio shuhudia tukio hilo wamesema kuwa baadhi ya watu walifariki katika mkanyagano uliotokea, baada ya polisi kutumia vitoza machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji hao.
Maelfu walikuwa wame jumuika mjini Bishoftu katika sherehe yakidini, eneo hilo liko umbali wa kilomita 40 kutoka mji mkuu Addis Ababa.
Maandamano hayo yame jiri masaa machache baada ya makesha kwa mshumaa yaliyo fanywa mjini Sydney na baadhi ya wanajumuiya wa Ethiopia wanao ishi nchini Australia, kwa kile wanacho sema kuwa ni kampeni ya vurugu inayo endeshwa na serikali nchini mwao.
Share
