Wiki ya maridhiano ya taifa ni wakati waku sherehekea naku jenga heshima kati yawa Aboriginal, wana visiwa wa Torres Strait na jamii pana ya wa Australia.
Katika wiki hii, tarehe muhimu katika historia yawa Australia wa asili huadhimishwa. Baadhi ya tarehe hizo muhimu ni kura ya maoni ya mwaka wa 1967 na uamuzi wa Mabo wa mwaka wa 1992.
Mandhari ya mwaka huu kwakimombo ni 'Let's take the next steps' au tupige hatua zinazo fuata, ambayo kwa baadhi ya watu mandhari hiyo ina maanisha kutambuliwa ndani ya katiba.
Share





