Siku hiyo huadhimishwa nchini Australia kwa sherehe tofauti pamoja na maandamano, yanayo ongozwa na wanaharakati wa jamii zawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, ambao ndiwo wa Australia wakwanza ambao wanataka tarehe hiyo ibadilishwe kwa sababu ya maovu ambayo wakoloni walifanyia jamii zao.
Dr Casta Tungaraza ni mwenyekiti wa bodi inayo toa ushauri wa maswala ya biashara na uhusiano, kati ya Australia na Bara la Afrika katika idara ya maswala ya kigeni ya serikali ya madola ya Australia. Dr Tungaraza pia ndiye mwanzilishi wa shirika la umoja wa wanawake nchini Australia.
Alishiriki katika ibada maalum ya tarehe 26 Januari, ambayo iliandaliwa na jamii yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait. Ibada hiyo ilipeperushwa katika runinga nchini Australia nakimataifa. Dr Tungaraza ali eleza SBS Swahili jinsi anahisi jamii yawa Afrika wanao ishi nchini Australia, wanastahili adhimisha siku kuu ya Australia (26 Januari).