Familia zinazo kabiliana na changamoto, zimesema misaada ya ziada, inastahili jumuishwa. Baadhi ya misaada wanayo taka nikupunguzwa kwa malipo ya huduma ya malezi yawatoto, na kuongezwa kwa likizo ya malipo ya wazazi katika bajeti ijayo.
Mweka hazina wa taifa Josh Frydenberg alieleza chama chakitaifa cha waandishi wa habari mwezi julai, kuwa njia bora yakupiga jeki viwango vya uzazi nikuhakikisha watu wana imani kuhusu siku za usoni za uchumi wa Australia.
Bw Frydenberg anajiandaa kutoa bajeti ya taifa tarehe 6 Oktoba 2020.