Hata hivyo chama cha Labor kina sisitiza kuwa gharama zina endelea kuongezeka, na sera hazi fanyi kazi licha ya uchumi unao chochewa na faida za ajira pamoja na bei za juu za bidhaa zina saidia kuboresha msingi, kupanda kwa mfumuko wa bei na sintofahamu kimataifa zinazo zua changamoto.
Wakati gharama za maisha zinaendelea kuongezeka, kufanya bajeti kwa vitu mhimu kuna endelea kuwa vigumu. Wateja wanaendelea kuhisi maumivu mfukoni kuanzia katika soko la vyakula hadi kwenye vituo vya kuuza petroli.
Wakati kitabu cha serikali kitakapo kuwa wazi, itakuwa jukumu la chama cha Labor kujibu. Na utakuwa ni mjadala wakiuchumi utakao dumu hadi wakati wa uchaguzi mkuu wa Mei 2022.