Kwa upande wa pili wa kampeni hizo za rais, Joe Biden ameongoza kwa muda mrefu katika kura za maoni kwa anaye tarajiwa kutangazwa mshindi.
Hata hivyo wanachama wa Democrats wana endelea kuwa na matumaini ya tahadhari baada ya miaka minne iliyopita kushuhudia mgombea wa Hillary Clinton kushindwa katika kura muhimu yakuunda serikali, licha yakushinda kura nyingi zaidi. Hali ambayo imewaachi wengi wakijiuliza kama radi yauchaguzi mkuu itagonga kwa mara ya pili nchini humo.
Ali Badawy ni mhariri katika redio ya The One Mic Show, ambayo hupeperusha makala yake mtandaoni kutoka Marekani. Bw Badawy alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi kampeni hizo zimekuwa nchini Marekani, pamoja na hisia kwa ujumla zawapiga kura kutoka pande zote zakisiasa nchini humo.