Moja ya madhara vizuizi hivyo vilisababisha nikufungwa kwa sehemu za ibada, hatua ambayo iliwaacha waumini pamoja na viongozi wakidini, wakitafuta mbinu mbadala zakuendelea kuabudu pamoja.
Mmoja wa watu walio kabiliwa na changamoto hiyo ni Mchungaji Melphon Mayaka kutoka kanisa la Uwezo LIberty Church. Katika mazungumzo maalum na idhaa ya Kiswahili ya SBS, Mchungaji Mayaka aliweka wazi changamoto ambazo yeye pamoja na waumini wake wame kuwa wakikabili kwa sababu ya COVID-19.
Kama unataka fuatilia ibada na mahubiri ya Mchungaji Mayaka, tembelea ukurasa wa Facebook wakanisa la Uwezo Liberty Church.