Bw Tim Mudasia ni mtaalam wa maswala ya fedha na mifumo ya benki, katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Mudasia aliweka wazi jinsi mfumo wa SWIFT unavyo tumiwa na umuhimu wake kwa mifumo ya benki.
Bw Mudasia alitoa mifano kadhaa kuhusu baadhi ya nchi ambazo ziliwahi pigwa marufuku kutumia mfumo wa SWIFT, na hatma ya uchumi wa nchi hizo baada ya miezi yakuwa chini ya vikwazo hivyo. Bw Mudasia alizungumza pia kuhusu madhara ya vikwazo hivyo vipya kwa biashara yakimataifa, hususan kwa mataifa ambayo yamekuwa washiriki wa Urusi katika biashara.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.