Ina aminika wagombea wanne wata wania wadhifa huo, katika mkutano wa chama Juma nne ijayo kumchagua kiongozi mpya.
Chama cha Liberal kinapo endelea kukabiliana na mshtuko wa tangazo lakujiuzulu la Gladys Berejiklian, hapajakuwa uhaba wa wanachama ambao wamejipendekeza kurithi kazi yake.
Yeyote atakaye chukua udhibiti wa chama na serikali ya NSW, itabidi aanze kazi kwa kasi akisawazisha matarajio ya ongezeko ya kesi za COVID-19, pamoja na mfumo wa afya ambao uko chini ya shinikizo kubwa, na malengo thabiti kwa ramani yakuondoka katika amri yamakatazo yakubaki ndani.