Shane Warne alikuwa na nafasi yakipekee katika historia ya mchezo wa Cricket, na wachambuzi wengi kwa mashabiki wame jadili kwa upana na urefo alivyo leta hamasa na uvutio katika mchezo huo.
Bw Warne alizua gumzo ndani ya uwanja kwa umahiri wake, lakini ni nje ya uwanja ndipo alizungumziwa zaidi kupitia matukio ya mara kwa mara yaliyo mhusu. Hata hivyo, matukio hayo yalichangia kwa ku kuwa kwa nyota yake ndani na nje ya mchezo huo wa Cricket, na mashabiki wengi walifuatilia matukio hayo kwa karibu kila mara.
Katika makala maalum, mchambuzi wa michezo wa SBS Swahili Herbert Gatamah, alitufafanulia kiwango cha ushawishi wa Shane Warne nje na ndani ya uwanja wa mchezo wa Cricket.