Je mataifa ya bara la Afrika, yana nufaikaje kupitia mikataba hiyo, na muhimu zaidi manufaa hayo yanawafikia raia wa nchi husika barani Afrika?
Dr Casta Tungaraza ndiye mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya maswala ya biashara pamoja na uhusiano yawananchi kati ya Australia na Afrika. Bodi hiyo inafanya kazi chini ya uongozi wa wizara ya mambo ya nje na biashara ya Australia.
Dr Tungaraza alieleza Idhaa ya Kiswahili, utaratibu unao tumiwa kufikia mikataba hiyo na jinsi nchi husika zinavyo faidi kupitia makubaliano yanayo afikiwa.