Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC imemkuta Ongwen na hatia ya makosa 61 kati ya 70 ya uhalifu ikiwemo mauaji, ubakaji, utumwa wa ngono, ndoa za kulazimisha, utekaji nyara watoto na kuwaandikisha kama wapiganaji, utesaji na mauaji. Ongwen amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.
Je! umeridhishwa na hukumu aliyopewa Dominic Ongwen?

Kamanda wazamani wa waasi wa Uganda Dominic Ongwen, asikiza mashtaka dhidi yake ndani ya mahakama ya jinai. Source: AAP
Kamanda wa zamani wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army nchini Uganda, LRA Dominic Ongwen amekutwa na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Share