Moja ya swala ambalo mara nyingi huwa halijadiliwi katika wakati wamakumbusho wa mauaji hayo, ni baadhi ya jamii yawa Hutu walio weka maisha yao hatarini kwa kuwaficha wa Tutsi waliokuwa wakisakwa wakati wa mauaji yakimbari nchini Rwanda.
Punde baada ya ibada hiyo, SBS Swahili ilizungumza na mmoja wa wanachama wajamii hiyo, aliye funguka kwa mapana na marefu kuhusu ibada hiyo pamoja na matukio wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.