John Kamau ni afisa wa umma katika shirika la KASA, shirika hilo huwakilisha nakuwahudumia watu wenye asili ya Kenya wanao ishi Kusini Australia.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifunguka kuhusu sera za vyama tofauti zilizo washawishi baadhi ya wanachama wa shirika lake walipo ingia ndani ya vituo vyakupigia kura siku ya uchaguzi mkuu.