Marehemu Daniel Toroitich Arap Moi ambaye alikuwa Rais wa pili wa Kenya, alikuwa na uhusiano wakipekee na waandishi wa habari, pamoja na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikipeperusha taarifa za habari nchini Kenya.
Linus Kaikai ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu katika kituo cha runinga cha Citizen nchini Kenya. Alifafanulia Idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi vyombo vya habari vilivyo fanya kazi chini ya utawala wa Moi, mivutano iliyo ibuka pamoja na jinsi ilivyo tatuliwa pamoja na jinsi marehemu Moi, alivyo heshimu taasisi nakutambua kuwa sehemu ya kazi ya waandishi wa habari, ilikuwa kuikosoa serikali miongoni mwa majukumu mengine.
Risala za rambi rambi zinaendelea kutumwa nchini Kenya kutoka mataifa mbali mbali kufuatia kifo cha rais mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi, na atazikwa nyumbani kwake Kabarak nchini Kenya.