Waziri Mkuu Anthony Albanese anatarajiwa kutembelea maeneo yaliyo athiriwa kwa mafuriko, kujionea kiwango cha janga hilo yeye mwenyewe.
Mvua kubwa na upepo mkali hatimaye vimepungua baada ya siku kadhaa za kuponda maeneo ya kaskazini ya Queensland, juhudi za usafi zime anza pole pole.
Kimbunga Jasper kime acha janga katika eneo hilo, ambako zaidi ya jumuiya 30 zime achwa zikiwe zimetengwa kwa sababu ya viwango vya juu vya maji ya mafuriko pamoja na uharibifu ulio sababishwa katika barabara.