Kiptum alivunja rekodi ya Eliud Kipchoge ya masaa 2:01:09 aliyo iweke mjini Berlin, Ujerumani.
Masaa machache baada ya historia hiyo kutengezwa, SBS Swahili ilzungumza na mwanariadha mstaafu kutoka Kenya ambaye kwa sasa ni mkaazi wa mji wa Perth, Magharibi Australia Bw Alfred 'Sergent' Koech.
Bw Koech alifunguka kuhusu historia ya wakenya katika riadha, pamoja na matarajio mapya kwa Bw Kiptum ambaye kwa umri wa miaka 23 wengi wana hisi ata endelea kuvunja rekodi nyingi.