Hata hivyo, Kenya haija wahi wakilishwa katika michuano hiyo, licha ya jamii hiyo kuwa na vijana wengi wenye uwezo mkubwa waku cheza soka.
Hatimae baada ya miaka mingi yaku hojiwa kwa nini Kenya haiwakilishwi katika michuano hiyo, vijana wa Kenya wametoa jibu hilo kwa kusajili timu yao, na masaa machache yajao Kenya itaingia dimbani dhidi ya Burkina Faso katika michuano ya Kombe la Afrika mjini Sydney, Australia.
Katika mazungumzo maalum katika hafla ya uzinduzi wa michuano hiyo, nahodha wa timu ya Kenya Bw Abed, alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi kikosi chake kimejiandaa pamoja na matarajio wanayo wanapo anza safari yao katika michuano hiyo.
Mechi ya Kenya ita anza saa saba mchana tarehe 7 Novemba 2020, katika uwanja wa Progress, South Granville, New South Wales, Australia.