Hatimae timu hiyo ili ingia dimbani dhidi ya Burkina Faso katika mechi ya kwanza ya kombe la Afrika jijini Sydney, New South Wales Jumapili 15 Novemba 2020 mashabiki wao wakiwa na hisia pamoja na matarajio mseto.
Licha yakuanza mechi kwaku fungwa goli la mapema vijana hao, walikaza buti nakuonesha umahiri wao katika mechi hiyo iliyo tawaliwa na joto kali.
Punde baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, mashabiki, wachezaji pamoja na mwalimu wa Kenya walichangia maoni na hisia zao kuhusu mechi hiyo na Idhaa ya Kiswahili ya SBS. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.