Dkt Maggy Sikulu-Lord ni mtafiti na mchambuzi wa madhara ya wadudu wanaosababisha magonjwa kwa binadamu, katika kituo cha sayansi ya wanyama ndani ya chuo cha Queensland.
Utafiti wa Dkt Sikulu-Lord unalenga mbu, wenye umuhimu wa matibabu hususan mbu wanaosambaza malaria, homa ya dengue, Zika na homa ya njano.
Dkt Sikulu-Lord aliielezea idhaa ya Kiswahili ya SBS juu ya utafiti huo, katika mazungumzo maalum.
Share






