Mamlaka inayo simamia mawasiliano nchini Kenya imetumbukiza Kenya katika giza la taarifa ya habari baada yakuzima mitambo iliyo kuwa ikipeperusha matangazo ya runinga nchini kote.
Hatua hiyo ime jiri wakati muungano wa NASA ulikuwa ukiendelea na maandalizi ya kuwaapisha vinara wao katika bustani ya Uhuru.
SBS Swahili ilizungumza na mwandishi wa habari akiwa mjini Nairobi kuhusu matukio hayo.
Share






