Wakati siku hiyo haina dhana thabiti yakidini hapa, ni siku ambapo wa Australia huendeleza sherehe zao za Krismasi.
Maranyingi ni wakati wa familia kuchangia vyakula, kutazama mechi za kriket pamoja na kutazama mashindano maarufu ya boti kutoka Sydney hadi Hobart.
Kwa upande mwingine, wa Australia wengi hutazamia siku hiyo kuenda madukani kupata punguzo bora zaidi.
Boxing Day, husherehekewa Disemba 26, ni likizo ya umma nchini Australia na hufuata sherehe za krismas kwa wakristo wa magharibi.
Siku hiyo ina chimbuko lake katika historia ya Uingereza ambako, kitamaduni ilikuwa siku yakuwapa wafanyakazi wa huduma boxi za krismas.