Naibu kiongozi wa jimbo hilo Jeremy Rockliff amerithi wadhifa huo, baada yakuchaguliwa bila kupingwa ndani ya mkutano wa chama tawala asubuhi ya Ijumaa wiki hii.
Kiongozi mpya wa jimbo hilo anarithi changamoto yakusimamia janga la UVIKO-19, ongezeko ya kodi na bei za nyumba kote jimboni, na mfumo wa huduma ya afya ambao umelemewa.