Wiki ya pili ya kampeni ya uchaguzi wa shirikisho imeshuhudia viongozi wa vyama viwili vikubwa, wakikabiliana katika mjadala wakitaifa ambako hoja ya usalama wa taifa ilikuwa kipaumbele cha ajenda.
Sajili ya uchaguzi mkuu wa shirikisho, ilifungwa Jumatatu 18 Aprili 2022. Zaidi ya wa Australia milioni 17 wanastahiki kupiga kura, uchaguzi mkuu wa shirikisho utakapo fanywa 21 Mei 2022.