Baadhi ya watu walio poteza ajira zao wakati huu wa janga la Uviko-19 wame amua kuanza biashara zao ndogo ndogo, kuweza kumudu gharama za maisha na wengine ambao hawaja poteza ajira zao wametumia fursa zilizo jitokeza kupitia janga la Uviko-19 kuwekeza katika sehemu mbali mbali za biashara hapa nchini Australia na katika nchi zao za asili.
Shirika la KISWA ambalo huwa hudumia wakenya wanao ishi jijini Sydney, lili andaa kongamano maalum ambako wanajumuiya walishiriki katika mazungumzo na wataalam tofauti katika sekta ya biashara wa nchini Australia na Kenya. Mratibu wa kongamano hilo Bw George, alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS, umuhimu wa kongamano hilo na jinsi wanachama wali faidika kupitia taarifa waliyo pokea.