Wa Australia wame iga baadhi ya tamaduni za ulaya, wakati pia wame unda tamaduni zao zakipekee. Habari nzuri ni kwamba kuna njia tofauti zaku sherehekea Krismasi nchini Australia.
Makala haya yata chunguza jinsi baadhi yawa Australia husherehekea msimu huu wa sherehe.
Krismasi ni likizo yakidini inayo sherehekewa na wakristo duniani kote kuenzi kuzaliwa kwa Yesu Kristo 25 Disemba. Ni wakati wa familia, kutoa zawadi, kuchangia upendo na ukarimu na wengine.
Wakati bado ni likioz yakidini kwa wengi, wa Austrlaia wengi huwa hawa enzi kipengele cha kiroho. Wanaona likizo hiyo kama, njia yakuja pamoja na familia na marafiki, kustaarabu nakusherehekea.
Nchini Australia, sherehe za krismasi kawaida kufanyika mida ya chakula cha mchana 25 Disemba.
Kuna njia nyingi zaku sherehekea krismasi, kwa hiyo jisikie huru kuchanganya tamaduni za Australia nazako.
Kutegemea na familia, unaweza pata tamaduni mbali mbali kama, kalenda za ujio, ibada za usiku wa manane, tamasha ya nyimbo pamoja na kuwashwa kwa miti ya krismasi.