Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa pamoja na ma Rais Paul Kagame (Rwanda) na Yoweri Museveni (Uganda), walimkaribisha Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri yakidemokrasia ya Kongo kuwa mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika hafla hiyo Rais Kenyatta alizungumzia matumaini yake kwa mwanachama mpya wa Jumuiya hiyo, pamoja na jinsi wanachama wenza wataweza faidi kupitia muungano huo.