Ujio wa taifa hilo kutoka kanda ya Afrika ya Kati, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki umepokewa kwa hisia mseto, baadhi ya wanachama wakiwa na hofu kuhusu kuhamishwa kwa migogoro ya DRC katika EAC ila wanachama wengine wamezingatia zaidi fursa zinazo fuata ujumuishaji wa DRC katika EAC.
Bw Kumbuka ni mfanyabiashara na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yeye hufanya biashara zake kati ya Australia na EAC. Alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS manufaa ya DRC kukaribishwa katika EAC, pamoja na fursa zakibiashara ambazo raia wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo watakazo pata.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.