Baadhi wanapenda rangi na mbwembwe ya matukio ya Jummanne ya kwanza ya Novemba, wakati wakaaji wa Melbourne hupata fursa yakufurahia likizo ya umma.
Ila, wanaharakati wa ustawi wa wanyama, wanachukia tukio hilo. Jumanne ya kwanza ya November, huashiria wakati mhimu kwa wa Australia wengi.
Saa tisa kamili, mamilioni ya watu kote nchini, hutazama Melbourne Cup. Wakaaji wa Victoria, wana likizo ya umma inayo wapa fursa yaku jiburudisha wakati wa mashindano hayo.