Miezi mitatu ya mauaji ilishuhudiwa nchini humo miaka 25 iliyopita, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda, ambavyo vilidai maisha mengi pamoja nakufanya watu wengi kutawanyika nje ya nchi hiyo nakuwa wakimbizi.
Maadhimisho ya Jumapili ni mwanzo wa wiki nzima yamatukio, yenye lengo lakuwakumbuka walio uawa. Inakadiriwa kuwa idadi yawatu elfu 10 wali uawa kila siku na asilimia 70 ya watu kutoka kabila la wachache la watutsi wali uawa pamoja, na zaidi ya asilimia 10 ya watu nchini humo, kabla ya vita hivyo kumalizika mwezi Julai 1994.
SBS Swahili ilihudhuria ibada iliyo andaliwa na jamii yawanyarwanda wanao ishi NSW, Australia ambako walifanya maadhimisho ya miaka 25 ya mauaji hayo ya kimbari. Bofya hapo juu kusikiza mazungumzo tuliyo fanya na baadhi ya wahanga wa mauaji hayo pamoja na viongozi wa jamii hiyo.