Baadhi ya watetezi wamekaribisha hatua hiyo ila, wengine hawaja furahi na wana hofu hatua hiyo inaweza sababisha madhara ndani ya jamii.
Serikali itakuwa na kura zakutosha kupitisha muswada huo ndani ya nyumba ya wawakilishi. Wakati chama cha Greens kina pinga vikali matumizi ya kadi hiyo, kuna uwezekano wata piga kura pamoja na serikali, kwa hiyo chama cha Labor kita ihitaji tu mbunge mmoja huru aunge mkono muswada huo ndani ya seneti.
Serikali imesema mipango zaidi ya usimamizi wa mapato, itajadiliwa wakati mashauriano na jamii yana endelea.