Hata hivyo Seneta Van, amekana madai hayo dhidi yake.
Wakati huo huo Kiongozi wa upinzani Peter Dutton, sasa ame mfukuza Seneta Van kutoka chama cha Liberal baada ya shutma za ziada kutolewa dhidi yake.
Wakati wa mjadala ndani ya Seneti kuhusu madai ya ubakaji ya mfanyakazi wa zamani wa chama cha Liberal Brittany Higgins, Seneta Thorpe alitumia fursa ya bunge kutoa madai hayo bungeni.
Kama wewe au mtu unaye jua angependa zungumza kuhusu unyanyasaji wakijinsia, familia au unyanyasaji wa nyumbani piga simu kwa namba hizi: 1800RESPECT on 1800 737 732 au tembelea tovuti hii: www.1800RESPECT.org.au. Katika hali ya dharura piga simu kwa namba hii 000.