Masaa machache kabla yakusomwa kwa bajeti ya taifa, Bi Lucy Gichuhi ali apishwa ndani ya Seneti ya shirikisho, baada ya wiki kadhaa za vuta ni kuvute kati yawanasheria wake, na wanasheria wa serikali na chama cha upinzani ndani ya mahakama kuu.
Mvutano huo ulizuka baada ya aliyekuwa kiongozi wa chama cha Family First Bob Day kuvuliwa useneta wake na vyama vingine kuhoji uhakiki wa Bi Gichuhi kuhudumu kama seneta kwa sababu ya uraia wake.
Hata hivyo mahakama kuu iliamua Bi Gichuhi anastahili kuhudumu kama Seneta, na hatimae Jumanne aliapishwa kuwa Seneta mpya huru wa Kusini Australia baada yaku jiondoa ndani ya chama cha Family First siku chache kabla.