SBS Swahili ilihudhuria maadhimisho ya miaka 53 ya Jamhuri ya Kenya mjini Canberra, Australia ambako ilizungumza na Naibu Balozi wa Mh Munyasia Mwangangi.
Bw Mwangangi alizungumzia maendeleo ambayo Kenya imefanya katika sekta mbali mbali elimu ikijumuishwa.
Bw Mwangangi alizungumzia pia mchanga ambao Kenya, imetoa kuboresha uchumi wa mataifa jirani katika ukanda wa mashariki ya Afrika. Pia Bw Mwangangi aliwahamasisha wakenya wanao ishi Australia, waendelee kuwa mabalozi wema wa nchi yao.
Bonyeza hapo juu kusikia mahojiano.
Share
