Msimu wa majira ya joto katika pwani ya mashariki ya Australia, umetawaliwa kwa muundo wa hali ya hewa wa La Nina, ambao kwa kawaida hu husishwa na mvua nyingi.
Ila mafuriko hayo ya mvua kubwa, yamesababisha mafuriko yanayo tishia maisha, katika sehemu nyingi za kaskazini New South Wales na Kusini Mashariki Queensland. Miji na vitongoji imezama wakati baadhiya wakaaji wakiwa wame kwama juu ya paa za nyumba, na wengine wakitumia mitumbwi katika mitaa kukimbia nyumba zao waki elekea katika vituo vya uhamisho. Barabara na shule zimefungwa, na usafiri wa treni kufutwa.
Jeshi la Ulinzi la Australia lime itwa kutoa msaada wa uokoaji, wakati wakaaji wengi wa maeneo hayo, wana endelea kutoma ujumbe wakusaidia kwa haraka kwa shirika la waokoaji la SES kupitia mitandao yakijamii.