Hatimae SBS Swahili ilifika katika mgahawa huo kuji thibitishia sifa na maoni ambayo ilikuwa iki pokea mara kwa mara kutoka kwa wateja na wapenzi wa vyakula vya mgahawa huo.

Baadhi ya vyakula ambavyo vina uzwa katika mgahawa wa Mama Nitiliye, Goodna, Queensland Source: SBS Swahili
Bi Esther alitupokea nakutueleza kilicho mpa moyo waku anzisha mgahawa huo pamoja na mapokezi ya vyakula anavyo uza, na jinsi alivyo kabiliana na changamoto ya amri zakubaki ndani wakati wa kilele cha UVIKO-19 jimboni Queensland.