Mji wa Ingham ume tengwa kutoka upande wa kaskazini na kusini kwa sababu ya mafuriko yanayo endelea, yaliyo sababishwa na kimbunga cha tropiki Jasper, pamoja na mvua nzito ambayo ime athiri maeneo ya Kaskazini Queensland kwa siku kadhaa.
Imeripotiwa kuwa ukanda wa Kaskazini Queensland ume shuhudia kiwango cha mvua inayo nyesha kwa muda wa mwaka mmoja katika siku chache, kufuatia kimbunga cha tropiki Jasper.
Mvua inatabiriwa kuendelea kunyesha kwa angalau masaa mengine 24, viwango vya maji vikitarajiwa kuvunja rekodi za 1977.