Utafiti mpya umepata kuwa watu wengi wanao pokea malipo ya Newstart, wanachagua kuishi bila chakula na huduma zingine, ili waweze mudu maisha kwa dola 40 kila siku.
Utafiti huo umejiri wakati shinikizo linaendelea kuongezeka kwa serikali, iongeze kiwango cha mafao hayo yakutokuwa na ajira.
Viongozi wabiashara nao pia, wame toa wito kwa kiwango cha malipo ya Newstart, kiongezwe kwa sababu hatua hiyo itapiga jeki uchumi wa taifa.
Hata hivyo Bw Morrison amesema, makato ya kodi ya serikali ya mseto kwa, wanao pokea mapato ya nchini na wastan, yatafanya hivyo pia.
Share






