Watu wapatao 26 wame fariki baada ya mshambuliaji kuwa miminia risasi waumini waliokuwa kanisani katika eneo la Kusini Mashariki ya mji wa Texas.
Kisa hicho kime tokea katika kanisa la First Baptist katika mji wa Sutherland Springs, ambao uko kilomita 65 Mashariki ya mji wa San Antonio, wakati wa ibada ya asubuhi ya Jumapili.
Ime ripotiwa mshambuliaji ni mzungu mwenye umri wa miaka 26, alipatwa ame fariki kwa risasi ndani ya gari yake kilomita chache na sehemu ya shambulizi.
Gavana wa Texas amesema hilo ndilo tendo kubwa zaidi la shambulizi katika historia ya Texas.
Share






