Je! mfanyakazi anastahili fanya nini, wakati majukumu yakazi yake, yanageuka kuwa tisho kwa usalama au maisha yake?
Mh Dkt Luc Mulimbalimba, anaye wakilisha jimbo la Kivu Kaskazini katika Jamhuri yaki Demokrasia ya Kongo, alijipata katika hali tata, ambapo majukumu ya kazi yake yaliweka maisha yake hatarini kiasi kwamba ilibidi, aondoke nchini mwake kwa muda.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Mh Dkt Mulimbalimba aliweka wazi masaibu aliyo kabiliana nayo nakama atarejea nyumbani, kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa yawapiga kura wake.