Wanachama wa jamii hiyo wali vamiwa naku uawa kinyama usiku wa manane wa 13 Agosti, ndani ya kambi yawakimbizi ya Gatumba nchini Burundi.
Wanawake, watoto kwa wanaume walipigwa risasi, `baadhi walikatwa kwa mapanga na wengine hata kuchomwa kwa moto hadi kufa.

Wahanga wa tukio hilo, walijumuika mjini Brisbane, Jumamosi 13 Agosti ambako walishiriki katika ibada maalum, yakuwakumbuka wapendwa wao walio uawa.

Bw Moise ni mwenyekiti wa jamii yawanyamulenge wanao ishi Australia, ali eleza SBS Swahili ombi la jamii yake miaka 18 baada ya tukio hilo. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.