Orodha ya walio tuzwa mwaka huu, ni kubwa zaidi katika historia ya tuzo za Australia, na watu takriban mia mbili watakao pokea tuzo hizo mwaka huu, walizaliwa ng'ambo.
Wanaume wawili walio shiriki katika oparesheni ya uokoaji wa wavulana 12 pamoja na mkufunzi wao wa soka, katika mapango yaliyo kuwa yame furika nchini Thailand mwaka jana, walitangazwa kuwa wa Australia wa mwaka wa 2019. Dr Craig Challen na Dr Richard Harris ambao ni marafiki wa muda mrefu, walikuwa wanajiandaa kuenda likizoni, walipo pokea ombi lakusaidia katika oparesheni ya uokoaji wa timu hiyo ya soka.
Wawili hao waliporejea nchini, walipewa tuzo la Nyota ya Ujasari, ambayo ni tuzo ya pili kwa umuhimu ya ujasiri nchini Australia.Kwa watu wengi, tuzo hiyo ni tazamio baada ya miaka mingi ya huduma, nakutoa michango katika njia zao tofauti.Ila wanacho changia ni nia yaku toa mchango, kadri ya uwezo wao kwa jamii zao.