Wachambuzi wa siasa nchini Marekani wamedokeza kuwa waziri mkuu aliweka uhusiano wake binafsi, na rais wa marekani juu ya maslahi ya Australia katika mazungumzo yake kwa simu.
Taarifa hiyo ya Australia baadae ilitumwa kwa serikali ya marekani baada ya FBI, kuanza kufanya uchunguzi kuhusu udukuzi wa urusi kwa barua pepe za Hillary Clinton. Uchunguzi huo ulisaidia kuanzisha uchunguzi wa Mueller kuhusu viungo kati ya kampeni ya Trump na urusi. Bw Downer ali eleza shirika la habari la ABC kuwa, hana taarifa yoyote kuhusu mawasiliano ya hivi karibuni kati ya Bw Trump na Bw Morrison.
Kwa muda mrefu bw Trump amepuuza uchunguzi wa Mueller, nakudai kuwa ripoti ya mwisho ili baini hana kosa.